Jumatatu, Julai 28, 2014

SAKATA LA SHILOLE KUGOMBEA UBUNGE 2015 IGUNGA

STAA wa muziki wa mduara anayefanya vizuri, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, amesema anatarajia kugombea ubunge katika jimbo analotoka la Igunga mkoani Tabora katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, alisema yupo tayari kugombea ubunge katika jimbo hilo na kama Mungu akipenda, atakuwa mbunge wa jimbo hilo kwa ridhaa ya wananchi.
Baada ya Dk. Dalali Kafumu anayefuata ni mimi, mimi nalipenda jimbo langu na napenda maendeleo ya wakazi wa Igunga, wengi wanaoniona tangu nakua hadi sasa hivi wananijua vizuri
alisema.
Alisema wakazi wa Igunga wanamwambia hawapendi kumpa mtu mwingine jimbo lao, hivyo wanampa changamoto, na kwamba vitu viwili vya kwanza ambavyo atavifanya akiingia bungeni ni kutetea haki za wasanii na kuhakikisha vijana wa Igunga wanapata kazi.

0 comments:

Chapisha Maoni