Mwanadada ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki
wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, amekamatwa na polisi nchini China baada ya kubeba madawa ya kulevya.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita
baada ya kupitishwa kwa msako maalum wa kutokomeza biashara hiyo katika
viunga vya Mji wa Hong Kong, China.
Kwa mujibu wa chanzo chetu chenye maskani yake Hong Kong, Mbongo Fleva,
Juma Khaleed ‘Jux Vuitton’ na meneja wa msanii wa Bongo Fleva aitwaye
Mirrow, Petit Man nao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika
kuunganishwa kwenye oparesheni hiyo ya ukamataji wa waingizaji wa
madawa ya kulevya nchini China.
Ilidaiwa kwamba Winnie alijikuta mikononi mwa askari wa China akidaiwa
kubeba mzigo wa unga tumboni hivyo kukamatwa na kutembezwa mitaani
kuelekea kituo cha polisi.
Ilisemekana kwamba
Winnie ambaye ni msichana wa mjini Dar, alifanikiwa kupita vizuizi vyote
lakini kwa hali ilivyo kwa sasa nchini humo ndipo akajikuta akikamatwa
na kutembezwa mtaani kama mhalifu wa kivita.
Unaambiwa ilikuwa kama vita kwani polisi wa China huwa wana silaha za kutisha sana. Unajua Winnie alikamatwa kwenye mitaa ambayo kuna Wabongo wengi hapa Hong Kong
Ilidaiwa kwamba askari hao walipokea agizo maalum kutoka kwenye
kitengo cha kudhibititi madawa ya kulevya nchini humo kwani kwa sasa
nchi hiyo imechafuka kwa uingizwaji wa madawa ya kulevya, jambo ambalo
limeifanya serikali ya China ifanye oparesheni kubwa ya kuhakikisha
wanatokomeza wimbi hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni