Jumanne, Julai 29, 2014

WAGOMBEA TUCTA WAPEWA ONYO

Wajumbe wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), wametakiwa kujitambua na kujitathmini pindi wanapotaka kugombea nafasi mbalimbali katika shirikisho hilo hususani urais.

Rai hiyo ilitolewa na Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (Raawu) Mkoa wa Dodoma, Ramadhani Mwendwa ambaye pia katibu wa Tucta Dodoma, alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima kuhusu maandalizi na mwenendo wa mkutano mkuu na uchaguzi wa Tucta utakofanyika hivi karibuni.
Mwendwa alisema kuwa kwa sasa kuna utitiri wa watu ambao wamejitokeza kugombea nafasi ya urais wa Tucta kwa lengo la kuziba nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Rais, Juma Ayubu ambaye alistaafu kwa mujibu wa sheria.
Kuna kila sababu ya wale wote ambao wanataka kugombea nafasi hiyo kujitafakari kama kweli wana nia ya kuwatetea wafanyakazi au wana malengo ya kujinufaisha wao na kulinda masilahi ya wakubwa na wafanya biashara
alisema.
Aliwataadharisha wajumbe wa mkutano mkuu wa Tucta ambao unatarajiwa kufanyika August 4 hadi 5 mwaka huu, kuhakikisha wanakataa rushwa ambazo zitajitokeza kutoka kwa wagombea.

0 comments:

Chapisha Maoni