Jumanne, Julai 08, 2014

MAJIBU YA CIA BAADA YA KUDAIWA 2PAC YUKO HAI


Miezi miwili baada ya Suge Knight aliyekuwa mmiliki wa Death Row Records kudai Tupac yuko hai na amechill sehemu fulani akivuta sigara ya Cuba, CIA imetoa majibu kuhusu mahali alipo baada ya kuulizwa kupitia Twitter.
CIA wamejibu katika Tweet ya July 7, na kudai kuwa wao hawafahamu mahali ambapo Tupac yupo (kama kweli yuko hai).  

Tupac alifariki mwaka 1996 baada ya kupigwa risasi huko Las Vegas na hadi sasa uchunguzi wa kifo chake haujatoa majibu ya kuridhisha yanayoweza kusaidia kumkamata muuaji/wauaji, suala ambalo lilimfanya Suge Knight kuwarushia mpira CIA na kudai kuwa Tupac hakufa na kama angekufa (CIA) wangekuwa wamewakamata waliomuua.  
Why you think nobody been arrested if they said they the one killed Tupac. Because Tupac not dead. Tupac not dead, nigga. If he was dead they’d be arresting those dudes for murder. You know he somewhere smoking a Cuban cigar on an island somewhere.
Alisema Suge Knight, mmiliki wa Death Row Records, sehemu ambayo Tupac alikuwa akifanyia kazi.

0 comments:

Chapisha Maoni