Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema anatarajia kupata kikosi
cha vijana 20 anaowahitaji kuanzia wiki ijayo ili kujiandaa na msimu
ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mchakato wa kutafuta vijana watakaocheza Ligi ya vijana, ulianza muda
wa mwezi sasa, na amejipanga kutaja kikosi bora kitakachochanganyika na
kikosi kikubwa katika maandalizi ya Ligi Kuu.
Akizungumza na Fichuo Tz Blog, Mwambusi alisema wiki hiyo pia
wanategemea kutangaza kambi ya maandalizi, na kwamba uongozi wa klabu
utaweka bayana kama watajificha wapi kujifua kwa kutengeneza kikosi
hicho kiweze kuchukua ubingwa msimu ujao.
Tumeanza mchakato wa kupata timu bora ya vijana kwa muda mrefu kwa sababu nia yetu ni kuhakikisha tunashiriki Ligi ya vijana katika ushindani mkubwa, ili tuchukue makombe kote
alisema.
Mwambusi alisema msimu uliopita timu hiyo ya vijana haikufanya vizuri
sana katika mashindano ya kombe la Uhai, pengine ni kwa sababu walikuwa
ndio wanaanza kwa mara ya kwanza lakini sasa wataingia na makali kama
timu kubwa.
Tumeona tuwe makini katika kuangalia kikosi chenye uwezo, ndio maana kuna ambao waliocheza mwaka jana wanaweza wasionekane msimu huu, tunaendelea kuangalia kwa kulinganisha viwango vyao
alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni