Muungano wa wapinzani wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo umemtuhumu Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo kuwa anakiuka haki za
binadamu hususan waandishi wa habari.
Muungano huo ambao unajumuisha wapinzani wa kisiasa na kijamii wa
serikali ya Kinshasa umekosoa vikali utendaji wa Rais Joseph Kabila na
umemtuhumu kiongozi huyo kuwa ametenda jinai dhidi ya binadamu.
Muungano huo umeitaka jamii ya kimataifa kutayarisha mazingira ya
kufikishwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika Mahakama ya
Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa ajili ya kujibu mashtaka ya kutenda jinai
ikiwa ni pamoja na kuua waandishi habari na wanaharakati wa masuala ya
haki za binadamu.
0 comments:
Chapisha Maoni