Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa kutokana na hazina ya chakula
kilichopo hakuna mtanzania atakayekufa kwa njaa na kwamba serikali ina
uwezo wa kukabili dharula yoyote ya chakula itakayojitokeza.
Rais Kikwete ambaye amepata mapokezi makubwa mjini Songea ameyasema
hayo baada ya kuwasili kwa ziara yake ya siku saba mkoani Ruvuma baada
ya kukagua ghala la mahindi la hifadhi ya taifa ya chakula (NFRA) la
mjini Songea na kuzindua ghala jipya la lenye uwezo wa kuhifadhi tani
elfu tano za mahindi.
Kwa upande wake naibu waziri wa chakula na ushirika mheshimiwa
Godfrey Zambi amesema kuwa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula nchini
unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kudaiwa deni la zaidi ya
shilingi bilioni nne na watoa huduma mbalimbali.
Naibu waziri huyo amesema kuwa katika msimu wa ununuzi wa mahindi
wa 2013/2014 hifadhi ya taifa ya chakula (NFRA) ilinunua tani 216,617 za
nafaka na kwamba NFRA ina maghala 31 nchini yenye uwezo wa kuhifadhi
tani 241,000 huku lengo likiwa kuongeza maghala na kuongeza zaidi
ununuzi wa mahindi.
0 comments:
Chapisha Maoni