Mwanamuziki maarufu wa Marekani Justin Bieber amekiri kosa la kufanya uharibifu katika nyumba ya jirani yake.
Mahakama imemtaka alipe faini ya dola 80,900 na pia kufanya kazi ya jamii kwa muda wa miaka mitano.
Wapelelezi
walifanya msako kwa nyumba ya Bieber huko Calabasas Carlifonia
wakitafuta ushahidi uliompelekea kusababisha uharibifu huo na baada ya
msako huo rafiki mmoja wa Bieber alipatikana na mihadarati na kunaswa.
Kwa mujibu wa polisi, ushahidi huo wa video
ulionaswa nyumbani mwa Bieber ulionyesha Bieber akiwasalimu maswahiba
wake baada ya kurusha Mayai kwa nyumba ya jirani yake na kusababisha
uharibifu.
Mashtaka ya Bieber yangewekuwa mabaya zaidi iwapo uharibifu huo ungesababisha hasara inayozidi dola elfu ishirini.
Bieber atawekwa chini ya uangalizi wa polisi kwa muda wa miaka miwili na iwapo ataonyesha mabadiliko atawachwa huru.
Mahakama pia ilitoa uamuzi kuwa Bieber apate
mafunzo ya kudhibiti hasira, kikamilifu. Bieber ambaye anakabiliwa na
mashtaka mengine mawili ya uhalifu huko Florida na Toronto, hakufika
mahakamani uamuzi huu ulipotolewa.
Mawakili wake walisema kuwa
Bieber amefurahi kuwa jambo hilo limesuluhishwa na ataendelea kusonga
mbele na kuwa makini katika kazi yake ya muziki.
Tangu kisa hiki Bieber alihamia Beverly Hills kutoka Calabasas.
Uchunguzi wa hapo awali uliojaribu kufuatilia
tabia za Bieber haukumpata Bieber na makosa ambayo yangepelekea
kumfungulia mashtaka yoyote.
Waendesha mashtaka mahakamani walikana
kumfungulia mashtaka mwaka uliopita baada ya jirani yake kulalamika kuwa
mwezi Novemba 2012 Bieber aliendesha gari bila kujali na kupita eneo
asilopaswa.
Hayo yakijiri, Bieber pia alishtakiwa huko Miami
kwa kuendesha gari akiwa mlevi na bila lessen halali. Kesi hiyo
itasikilizwa baadaye mwezi huu. Aidha, katika msururu huo wa kesi,
Bieber ameshtakiwa kushambulia dereva mmoja mnamo mwezi Disemba huko
Toronto.




0 comments:
Chapisha Maoni