Jumatatu, Juni 30, 2014

WANAWAKE WATANZANIA WABAKWA INDIA

Wanawake wawili wa Kitanzania wanadai kubakwa na wanaume wawili kusini mwa Delhi katika eneo linalojulikana kama Sarojini Nagar. Kwa mujibu wa polisi wa huko, inadaiwa kuwa wanawake hao walio kwenye late 20s walibabwa jana Ijumaa na wanaume wawili waliotajwa kama Satish Singh (27) na Kunal (28) kwenye nyumba moja eneo la Sarojini Nagar.
Baada ya kupokea simu, polisi waliwasili eneo la tukio na kuwakuta wote wanne wakiwa kwenye chumba kimoja. Wanaume hao wawili walikamatwa baada ya wanawake hao kuchukuliwa maelezo huku wakidai kuwa wamebakwa na wanaume hao.
Wameiambia polisi kuwa wanaume hao waliwapeleka kwenye chumba hicho na kuwabaka. Polisi wamedai kuwa wanawake hao walikuwa wanawafahamu wanaume hao na kwamba kulikuwa na mabishano baina yao juu ya suala dogo kabla ya wanawake hao kuwapigia polisi. Wanaume hao wamefikishwa mahakamani hivi leo na kurudishwa mahabusu.

0 comments:

Chapisha Maoni