Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius hakuwa na tatizo lolote la kiakili wakati alipomuua mpenzi wake mwaka jana.
Haya ni matokeo ya uchunguzi wa kiakili aliofanyiwa Oscar Pistorius huku kesi yae ikianza kusikilizwa tena nchini Afrika Kusini.
Ripoti hiyo iliwasilishwa baada ya uchunguzi kufanywa kuhusu hali yake ya kiakili wakati alipofanya mauaji hayo mwaka jana.
Mawakili wake walikuwa wamedai kuwa Pistorius
aliukuwa anakumbwa na hali ya wasiwasi na kuzongwa na mawazo wakati wa
mauaji ya Reeva Steenkamp.
Mwanariadha huyo amekana kumuua kwa maksudi
mpenzi wake Reeva Steenkamp akisema kuwa alimpiga risasi kwa bahati
mbaya baada ya kupatwa na wasiwasi akidhani jambazi alikuwa amevamia
nyumba yake.
Upande wa mashitaka pamoja na utetezi wamekubali matokeo ya uchunguzi huo.
Upande wa utetezi sasa unasikia ushahidi wake
daktari aliyemkata miguu Pistorius, Gerry Versfeld, anayetoa ushahidi
kuhusu athari za Pistorius kukatwa miguu.
Upande wa utetezi nao unatarajiwa kumaliza ushahidi wake katika siku chache zijazo.
Bi Steenkamp, alikuwa na umri wa miaka 29, wakati wa mauaji yake Februari mwaka jana.
0 comments:
Chapisha Maoni