Jumatatu, Juni 30, 2014

SUAREZ AKIRI KUNG'ATA, AOMBA RADHI

Luis Suarez amuomba radhi Chiellini
Katika taarifa yake kwenye twitter amesema hivi:
Baada ya siku kadhaa za kuwa nyumbani na familia yangu, nimekuwa na muda wa kutulia na kutafakari kuhusu hasa kilichotokea wakati wa mchezo kati ya Italy na Uruguay Juni 24 2014.
Mbali na taarifa na zilizozagaa katika siku chache zilizopita, ambazo nyingi zimekuwa hazina nia ya kutatiza uwezo mzuri wa timu yangu ya taifa, ukweli ni kuwa, mwenzangu Giorgio Chiellini aliumia kutokana na mimi kumng'ata kutokana na kugongana na mimi. Kwa hilo:
*Nasikitika sana kwa kilichotokea.
*Ninamuomba rahi Giorgio Chiellini na familia yote ya wanasoka
*Naahidi watu wote kuwa hakutakuwa na tukio kama hili tena

0 comments:

Chapisha Maoni