Serikali ya Sierra Leone imeonya kuwa ni hatia kumpa hifadhi mtu yeyote aliyeambukizwa virusi vya Ebola.
Hii ni baada ya taarifa kuwa baadhi ya wagonjwa wametoroka hospitalini na kujificha.
Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini
humo, baadhi ya wagonjwa wa homa hiyo kali wametoroka hospitalini katika
wilaya ya Kenema, kitovu cha mlipuko wa ugonjwa huo.
Shirika la afya duniani, WHO, limetoa wito wa
hatua za haraka kuchukuliwa kudhibiti homa hiyo katika kanda ya Afrika
Magharibi ambapo hadi sasa wagonjwa 400 wamefariki.
Mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo ndio mkubwa zaidi
kushuhudiwa hasa kwa kuwa umesabaisha vifo vingi na kuenea zaidi katika
nchi nyinginezo za kanda hiyo.
Visa zaidi ya 600 vya ugonjwa huo vimeripotiwa
nhini Guinea ambako ulianza miezi minne iliyopita na katika mataifa
jirani ya Sierra Leone na Liberia.
Takriban asilimia 60 ya watu walioambukizwa ugonjwa huo wamefariki.
Shirika la afya duniani linasema kuwa watu 46 wako katika hali mahututi kati ya 176 walioambukizwa ugonjwa huo.
0 comments:
Chapisha Maoni