Manchester United huenda wakawazidi kete Chelsea katika kumsajili Cesc
Fabregas, kwa kuwa hawachezi Champions League msimu ujao, Barcelona
wanaona hawatakuwa mahasimu wao wa moja kwa moja (Daily Express), hata
hivyo Chelsea wako tayari kumpa Fabregas pauni LAKI MBILI kwa wiki ili
kumshawishi kwenda Darajani (Metro), Liverpool wapo tayari kuacha
kumsaka Adam Lallana, na kuelekeza nguvu zao kwa Lazar Markovic wa
Benfica, na kuna taarifa kutoka Lisbon kuwa huenda
mkataba huo ukaafikiwa kwa pauni milioni 25 (Daily Mirror), Tottenham
wamepanda dau kumsajili beki wa kushoto wa Sevilla, Alberto Moreno,
ambaye pia anasakwa na Liverpool. Spurs wametoa pauni milioni 14 pamoja
na kiungo wao Etienne Capoue na Roberto Soldado- kwa mkopo (Daily Mail),
Romelu Lukaku anatakiwa na Atlètico Madrid kwa mkopo ili kuziba pengo
la Diego Costa, lakini Valencia wapo tayari kutoa pauni milioni 18
kumchukua jumla (Daily Mirror), Arsenal wanamfuatilia beki Nemanja
Pejcinovic ambaye hana mkataba kwa sasa baada ya kuondoka Nice ya
Ufaransa (Daily Express), Schalke ya Ujerumani na Al Ain ya Imarati
zinamnyatia Joleon Lescott wa Manchester City (Sky Sports), Carlos Vela
amehusishwa na kurejea Arsenal, lakini huenda akajiunga na Real Madrid
(ESPN), Barcelona wapo tayari kutoa hadi pauni milioni 56 kumsajili
Sergio Aguero kutoka Manchester City (Daily Star), vyanzo mbalimbali vya
habari vinadai kuwa Diego Costa wa Atlètico Madrid tayari amefanya
vipimo vya afya Chelsea na yuko tayari kujiunga rasmi na Blues kwa pauni
milioni 32. Arsenal huenda wakatumia makubaliano ya kumnunua tena
yaliyopo kwenye mkataba wa Carlos Vela, ili arejee Emirates (The Sun),
Mario Balotelli anajiandaa kuondoka AC Milan na kujiunga na Galatasaray
(Milliyet)
0 comments:
Chapisha Maoni