Alhamisi, Juni 05, 2014

KITU CHA AJABU KUHUSU MPIRA UTAKAO TUMIKA KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Mpira rasmi utakaotumika katika michuano ya Kombe la Dunia unaitwa "Brazuca." Maana yake ni "Ya Kibrazil" ikimaanisha mienendo ya kimaisha ya Brazil. Mpira huo utatengenezwa na kampuni ya Adidas, ambao ndio watengenezaji rasmi wa mipira ya Kombe la Dunia tangu mwaka 1970.
Huu ni mpira wa kwanza kabisa kupewa jina na mashabiki, baada ya kura kupigwa na mashabiki zaidi ya milioni moja nchini Brazil. Jina "Brazuca" lilipata asilimia 77.8 ya kura zote. Majina mengine yaliyopigiwa kura ni "Bossa Nova" ambao ni mtindo wa muziki na "Carnavalesca" ambayo ni Carnival.
Mpira wa Brazuca unatengenezwa na vipande sita vya aina ya mpira ujulikanao kama polyurethane ambao huufanya mpira huo kutoingia maji, na tipu lake (yaani mpira wa ndani) linatengenezwa na mpira wa latex, ili kutoa mdundo bora kuliko mipira mingine iliyowahi kutengenezwa awali.
Pia "Brazuca" unadaiwa kuwa na uwezo mzuri zaidi wa kuelea angani kuliko "Jabulani" uliotumika Afrika Kusini mwaka 2010.

0 comments:

Chapisha Maoni