Serikali
ya CHINA imekabidhi msaada wa gari la kisasa la kurushia matangazo ya
nje ya televisheni kwa Shirika la Utangazaji TANZANIA, TBC, lenye
thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni SITA.
Akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa gari hilo jijini DSM, Makamu wa Rais wa CHINA, LI
YUCHUAN amesema msaada huo unalenga kudumisha uhusiano mwema kati ya
nchi hizo mbili na kuongeza kuwa serikali yake inaamini kuwa utatumika
kuwaunganisha Wachina na Watanzania kupitia vipindi mbalimbali katika
Nyanja za Uchumi, Elimu, Sayansi, Teknolojia na Utamaduni.




0 comments:
Chapisha Maoni