Alhamisi, Juni 05, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Siku kama ya leo miaka 47 iliyopita muwafaka na tarehe 5 Juni 1967, vilianza vita vikubwa vya tatu kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na nchi za Kiarabu. Katika siku kama ya leo kikosi cha anga cha utawala ghasibu wa Israel kilifanya shambulizi la kushtukiza na kuvuka mipaka ya nchi tatu za Misri, Syria na Jordan na kufanya uharibifu mkubwa. Baada ya shambulizi hilo, vikosi vya nchi kavu vya Israel vikiwa na silaha za kisasa na uungaji mkono wa Marekani na Uingereza, vilifanikiwa kuyashinda majeshi ya Misri, Syria na Jordan katika kipindi cha siku sita tu.

0 comments:

Chapisha Maoni