Siku kama ya leo miaka 42 iliyopita, sawa na tarehe 5 Juni 1972,
lilifanyika kongamano la kwanza la mazingira huko Stockholm nchini
Sweden. Kongamano hilo liliwashirikisha wawakilishi 1300 kutoka nchi 113
duniani likiwa na kauli mbiu isemayo 'Kuna Ardhi Moja tu'. Miongoni mwa
malengo makuu ya kongamano hilo yalikuwa ni kuwekwa mikakati ya kujenga
makaazi ya raia kwa kuzingatia ulindaji mazingira, kuainisha na
kudhibiti mada haribifu kwa mazingira na kuhifadhi mazingira kwa ajili
ya vizazi vya baadaye.
0 comments:
Chapisha Maoni