HATIMAYE familia ya denti wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, marehemu Sekabenga Pius Mwakimenya (21) kilichotokea hivi
karibuni na kugubikwa na utata, imeanika ukweli kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili, baba mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la
Joseph Mwigune alisema, taarifa waliyopewa na daktari aliyemfanyia
uchunguzi inamaliza utata na minong’ono yote inayoendelea chuoni.
Alisema, kwa mujibu wa ripoti hiyo, kifo cha Sekabenga kimetokana na
mzunguko wa damu katika mishipa kutokuwa sawa, jambo lililosababisha
ajisikie vibaya na hatimaye kufariki dunia.
Daktari amesema kwamba mishipa ya damu haikuwa ikifanya kazi vizuri hali iliyomsababishia ajisikie kuchoka kwa sababu damu haikuwa ikifika sehemu zote za mwili wa marehemu
alisema Mwigune.
Chanzo kilifunga safari hadi chuoni na kuzungumza na baadhi ya
wanafunzi ambao walionyesha wasiwasi kuwa huenda marehemu aliamua kujiua
kwa sumu kwa maelezo kuwa, siku chache kabla ya kifo chake alionekana
mwenye mawazo mengi.
Hakuwa mwenye furaha, ni kama alikuwa na jambo zito linalomsumbua ndiyo maana unasikia wanafunzi wengi hapa chuoni wanahusisha kifo chake na sumu
alisema denti mmoja kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Hata hivyo, taarifa kutoka kwa familia inayonukuu ripoti ya daktari
inaziba minong’ono yote kwa kuwa haionyeshi mahali popote kuwa marehemu
alijiua kwa sumu.
Marehemu Sekabenga alikuwa mwaka wa pili chuoni hapo akichukua
Shahada ya Kwanza ya Biashara na Uhasibu, mwili wake umesafirishwa
Jumamosi Mei 31, mwaka huu kuja mkoani Mbeya kwa maziko yaliyotarajiwa
kufanyika jana Jumatatu.
0 comments:
Chapisha Maoni