Polisi nchini katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wamepiga marufuku
maandamano ya watu wanaowaunga mkono zaidi ya wasichana wa shule mia
mbili waliotekwanyara na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali za
kiislamu la Boko Haram mwezi Aprili.
Maandamano
yamekuwa yakiandaliwa kila siku kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja
kuishinikiza serikali kutia bidii zaidi katika juhudi za kuwakomboa
wasichana hao.
Polisi wanasema maandamano hayo yanamepigwa marufuku kwa kuwa yanazua hatari kwa wenyeji.
Aibu kwa serikali
Kampeini ya 'Bring back our Girls, au
warudisheni wasichana wetu,'' ambayo imekuwa ikifanywa nchini Nigeria na
hata nje ya Nchi hiyo imeleta aibu kubwa sana kwa serikali ya Nigeria.
Waandamanaji wamekuwa wakikutana hadharani
wakiishinikiza serikali hiyo kukoma kuzungumza tu katika vyombo vya
habari na badala yake waongeze jitihada na kuhakikisha wasichana hao
wamekombolewa.
makosa sio ya serikali
Lakini wiki iliyopita, kundi tofauti lilianzisha
kampeini sambamba, na hata kuvuruga ile ilyokuwa ikiendelea ambapo
wanadai kuwa hasira zinastahili kuelekezewa hao watekaji nyara na wala
sio serikali ya Nigeria.
Kundi hili linatumia nembo 'Release Our Girls Boko Haram'. Wameongeza jina Boko Haram kwa kusudi hapo mwisho.
Polisi sasa wanasema kuwa maandamano haya yanatishia usalama kwa wananchi wa Abuja.
Lakini waandamanaji wanaoendesha kampeini ya
'Bring Back our Girls' sasa wanaona kama hili ni jaribio la serikali
kuwanyamazisha na wamewasilisha ombi mahakamani kutaka kutolewe agizo la
kuvunja amri hiyo ili waruhusiwe kufanya maandamano yao.
0 comments:
Chapisha Maoni