Hii ilikua siku nyingine muhimu kwa Tanzania na Africa kwa ujumla
ambapo yalikua yanasubiriwa matokeo ya tuzo ya BET sanasana kipengele
wanachowania tuzo wasanii wa Afrika akiwemo Diamond Platnumz.
Davido kutoka Nigeria ndio amethibitisha kuwa mshindi wa tuzo hii
ambapo kupitia page yake ya Instagram amewashukuru mashabiki na kuelezea
furaha yake.
Tuzo hii ilikua inawaniwa na Diamond Platnumz kutoka Tanzania,
Mafikizolo wa South Africa, Sarkodie wa Ghana, Tiwa Savage wa Nigeria na
Toofan wa Togo.
Pamoja na kwamba Diamond hajawa mshindi wa tuzo hii, Watanzania wengi
wamekua upande wake toka alipochaguliwa kuwania tuzo hizi na kumwambia
hata kama hatoshinda, kuchaguliwa tu kushiriki BET ni zawadi ya kipekee
na hatua kubwa kimuziki.
Namkariri Rais Jakaya Kikwete pia aliesema ‘Hata kama asiposhinda
Diamond, yenyewe kuchaguliwa kwenye tuzo za BET ni hatua kubwa kimuziki’
0 comments:
Chapisha Maoni