Leo kabla ya kujadiliwa kwa bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii
ilianza sehemu ya maswali na majibu kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa
nne.
Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Juma Nkamia ndio alijibu
swali la Catherine Magige kuhusiana na udhalilishaji wa Wanawake
unaofanywa kwenye kumbi mbalimbali za starehe Tanzania.
Waziri Nkamia
alisema ‘nakubalia kabisa kwamba kumbi za starehe zimekua zikitoa
burudani na ajira kwa vijana hapa nchini lakini ndani ya kumbi hizo
kumekua na vitendo vinavyofanyika kinyume na maadili ikiwemo
udhalilishaji wa Wanawake’
Katika kukomesha hali hiyo serikali kupitia baraza la sanaa BASATA wamefanya vikao kadhaa na wamiliki wa bendi, maafisa utamaduni, wakuu wa polisi, wamiliki wa kumbi na wanaojihusisha na uchezeshaji wa mtindo wa kanga moja ili kujadili ukiukwaji wa maadili kwenye sanaa
Waziri amesema
Pia serikali imeacha kutoa usajili kwa vikundi kama cha kanga moko kwa kuwa uchezaji wake unakwenda kinyume na maadili ya Tanzania na kutoa onyo kwa wamiliki wa kumbi, Wasanii na hata asasi zinazojihusisha na sanaa ambazo hazifati maadili
Amesema
Wasanii waliopewa Onyo ni Ney wa Mitego, Shilole, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na kwa upande wa kumbi ni Mama’s and Papa’s lakini pia maonyesho ya urembo ya Miss Utalii yalifungiwa ambapo pia Serikali imeunda kamati ya kitaifa ya kuzuia ukatili na unyanyasaji dhidi ya Wanawake/Wasichana watoto
0 comments:
Chapisha Maoni