Serikali imepiga marufuku na kutaka kuondolewa mara moja mabango yote
ya wataalam wa tiba asili yanayojitangaza kutibu maradhi ambayo
hayajathibitishwa kitaalamu yaliyobandikwa maeneo mbalimbali nchini huku
baadhi ya wabunge wakitishia kukwamisha bajeti ya wizara ya fedha
endapo wizara hiyo haitatoa kiasi cha fedha cha zaidi ya asilimia 50 ya
bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii.
Wakichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya maji
mara baada ya waziri mwenye dhamana pamoja na kamati ya bunge na kambi
ya upinzani bungeni kuwasilisha maoni yao siku ya Jumamosi iliyopita
baadhi ya wabunge wamesema licha ya kuwa Tanzania ina maeneo ambayo
yanajulikana kuwa na matatizo makubwa ya maji kutokana na ukame bado
mawaziri hao wamejitengea kiasi kikubwa cha fedha kutekeleza miradi ya
maji licha ya kuwa maeneo hayo yanaunafuu ya upatikanaji wa maji pamoja
na idadi ndogo ya watu.
Pia baadhi yao wamezitupia lawama mamlaka za miji
za maji kwa kushindwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi huku
wafanyabiashara wa maji wanaotumia malori wakipata maji na kuwauzia
wananchi kwa bei kubwa huku baadhi yao wakidhamiria kutoa hoja binafsi
bungeni kujadili kauli ya waziri aliyoitoa bungeni kuwa tatizo la maji
jijini Dar es salaam limepungua.
Mara baada ya bajeti ya wizara ya maji kupitishwa
na bunge wizara ya afya na ustawi wa jamii hii leo nayo imewasilisha
hotuba ya bajeti yake bungeni mjini Dodoma.
0 comments:
Chapisha Maoni