Mganga wa Jadi raia wa Ghana, amedai kwamba anahusika kikamilifu kwa
jeraha la nahodha wa Portugal, Cristiano Ronaldo linalotishia ushiriki
wake kwenye Kombe la Dunia. Portugal wapo kundi moja Group G, kundi
gumu lililobatizwa jina la 'Kundi la Kifo', ambapo ukiachilia Portugal
yeyewe pia zimo timu za Germany, USA na Ghana yenyewe.
Ronaldo hajacheza mchezo wowote tokea alipofunga moja kati ya mabao
manne ya Real Madrid katika fainali ya Champions League dhidi ya
Atletico Madrid May 25 na taarifa iliyotolewa na Chama cha Mpira cha
Portugal siku ya Jumatano kimethibitisha kwamba straika huyo ana taabu
katika misuli katika goti lake la kushoto na pia kushikwa na misuli ya
paja.
Mganga huyo wa kienyeji, ambaye jina lake ni Nana Kwaku
Bonsam(pichani) likiwa na maana 'Jini la Jumatano', alitabiri Mwezi wa
Pili mwaka huu(Februari) kwamba Ronaldo atalazimika kulikosa kombe la
Dunia ili kuipa Ghana nafasi kubwa zaidi ya kupita katika "kundi hilo la
kifo".
Katika mahojiano na kituo cha habari cha Kumasi-kiitwacho
Angel FM, alijibu kwa kusema:
Najua kila kitu kuhusu jeraha la Cristiano Ronaldo, Na naendelea kumfanyia kazi.
Sina utani kuhusu hili. Wiki iliyopita, nilikua katika mizunguko nikitafuta mbwa wanne na niliwapata, nitawatumia kutengeneza dawa maalum ya nguvu za giza inayoitwa Kahwiri Kapam.
Nililisema hili miezi minne iliyopita kwamba nitamshughulikia Cristiano Ronaldo na nitahakikisha anakua nje ya Kombe la Dunia ama angalau kuzuia asicheze dhidi ya Ghana na njia pekee ya kufanikisha hili ni kumuweka nje kwa njia ya majeruhi.Jeraha hili haliwezi kutibika kwa dawa yoyote, na haitokua wazi nini hasa kinasababisha kwa sababu ni nguvu za giza. Leo watasema ni goti, kesho watasema ni paja, na siku itakayofuata watasema ni kitu kingine.
0 comments:
Chapisha Maoni