TANGU ilipoanza tasnia ya filamu nchini katika miaka ya 2000, unaweza
kujiuliza kwa nini hadi leo wanaomiliki filamu zao wengi ni wasanii wa
kiume.
Ingawa katika kuigiza filamu hizo, wanawake pia wanahusika kwa kiasi
kikubwa na kufanya filamu kupendeza na kuvutia, lakini katika kumiliki
ni wachache wanaozimiliki ingawa wameanza pamoja. Wasanii wengi wa kike
wanasema miongoni mwa sababu kubwa za kutomiliki filamu zao, kunatokana
na utumwa wa kingono wanaolazimishwa na wasambazaji, wadau na wasanii
wenzao.
Wengine wakidai kwamba uhaba wa fedha, ubabe kwa baadhi ya dairekta
na mpigapicha kunawafanya washindwe kufikia malengo yao. Miongoni mwa
wasanii ambao wamepata suluba kutoka kwa mpigapicha, ni mwigizaji Emmy
Sizya wakati anatengeneza filamu yake ya kwanza ya Tumaini langu.
Anasema filamu hiyo iliyoandikwa na rafiki yake, David pia ni msanii
aliyeshiriki kuigiza filamu hiyo.
Kabla sijaanza kuigiza, rafiki yangu aliniambia, kutengeneza filamu kuna changamoto nyingi. Hasa kwa mtoto wa kike ndo balaa
anasema
Sizya.
Anasema alikubaliana kupokea changamoto zote zitakazojitokeza, ndipo
akaanza maandalizi ya filamu hiyo mwaka 2012 huku akimteua Kulwa Kikubwa
kama mwongozaji wa filamu hiyo.
Nilianza filamu nikiwa na mtaji wa kutosha kuweza kukamilisha mapema na kuweza kuingiza sokoni
alisema na
kuongeza kuwa hakupata tabu katika kuhakikisha anapata wasanii kwa
ajili ya filamu yake, kuwalipa kulingana na kazi waliyokuwa wakiifanya.
Anasema tatizo likaja baada ya kukamilika filamu hiyo, ndipo usumbufu
ulipoanza kuchomoza. Filamu iliisha mapema kama ambavyo alifikiria,
lakini anasema baada ya kukamilika, ndipo mpigapicha aliposafiri bila ya
kukamilisha kazi hiyo. Anasema ni kawaida sana wapigapicha wa filamu za
Tanzania kuchukua kazi zaidi ya moja, mbabe ndiye anaweza kupewa kazi
yake haraka hata kama atakuwa wa mwisho.
0 comments:
Chapisha Maoni