Jumapili, Mei 11, 2014

WANAFUNZI ZAIDI YA 1500 HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA KATAVI

Mkoa wa katavi unakabiliwa na tatizo kubwa la kuwa na watoto zaidi ya 1,500 wasiojua kusoma na kuandika, kwenye shule zake za msingi mbalimbali, na huku mdondoko (Drop outs) ukifikia zaidi ya asilimia 40 kwa shule za msingi na zile za sekondari, hali inayosababisha watoto wengi kushindwa kumaliza masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na malezi yasiyo sahihi.

0 comments:

Chapisha Maoni