Jumapili, Mei 11, 2014

SHULE ALIYOFUNDISHA MWL. NYERERE (PUGU) YAVAMIWA NA KUNGUNI!!!

SHULE ya Sekondari ya Pugu, iliyopo maeneo ya Pugu jijini Dar es Salaam, ambayo inasifa kubwa nchini kwa kuwa iliwahi kufundishwa na Baba wa Taifa, hayati Julius Kambarage Nyerere, imevamiwa na wadudu aina ya kunguni ambao wanadaiwa kuwasumbua wanafunzi wa bweni wa shule hiyo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Agustino Angelo, alisema tatizo hilo limekuwepo muda mrefu na wamejitahidi kulipunguza kwa kiasi kikubwa kwa kufanya upuliziaji (fummigation) mara mbili huku naye Mstahiki Meya wa Ilala Jerry Slaa, akiahidi kulimaliza kabisa tatizo hilo katika siku za hivi karibuni.
Chanzo chetu kilizungumza baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, ambao walikiri kusumbuliwa na tatizo hilo ambalo wanadai kuwa linawakosesha amani na kuwataka viongozi wa serikali wajitokeze kutokomeza tatizo hilo ili waendelee na masomo yao vizuri.
Aidha chanzo kilishuhudia majengo chakavu ya shule hiyo, mazingira ambayo si rafiki na heshima ya shule hiyo yenye historia kubwa nchini kana kwamba shule hiyo imesahaulika.

0 comments:

Chapisha Maoni