Mume (bado talaka) wa mwanamitindo maarufu Bongo ambaye kwa sasa yuko
korokoroni Macau nchini China kwa msala wa kukamatwa na unga, Jacqueline
Fitzpatrick Cliff, Abdulatif Fundikira ‘Tifu’ anadaiwa kumnasa kimalavu
Miss Tanzania 2011, Salha Israel.
Tifu na Salha Israel Kifai |
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Tifu, wawili hao hivi sasa wako
kwenye ‘mahaba niue’ na wote wawili wako tayari kufunga ndoa kwani
wazazi wa pande zote wamebariki ndoa hiyo.
Salha sasa hivi humwambii kitu kwa Tifu na kila mmoja yuko tayari kwa ajili ya kufunga ndoa na mwenzake. Lakini sisi kama marafiki wa karibu tunaona ni jambo la heri
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa huko nyuma Tifu alikuwa hana
imani kabisa na wanawake tena baada ya kuingia kwenye mgogoro mzito na
aliyekuwa mke wake, Jack Patric, kiasi ambacho alisema hawezi kuoa tena.
Rafiki huyo alisema kuwa baada ya Tifu kukutana na Salha aliona ndiye
anaweza kuwa mke bora (wife material) na kuamini kuwa hawezi kumtenda
kama alivyofanyiwa huko nyuma.
Baada ya kupata taarifa hizo, Fichuo Tz ilimtafuta Tiff ili kupata
ukweli wa madai hayo ambapo bila kukanusha alisema kuwa ni mapema
kulizungumzia hilo kama yatakuwa tayari ataweka wazi.
Salha Israel Kifai |
Kwa kweli hilo jambo ni mapema mno kulizungumza kwa hivi sasa lakini mambo yakikuwa tayari nitaweka wazi kila kitu
alisema Tifu.
Kwa upande wake Salha Israel alipopatikana kwa njia ya simu alifunguka:
Ni kweli namfahamu, ni mtu wa karibu lakini ni sawa na kaka yangu pia. Hayo mengine labda mumuulize yeye.
0 comments:
Chapisha Maoni