Muigizaji mashuhuri wa Hollywood nchini Marekani,
Shailene Woodley, mapema wiki hii aliwashangaza watu alipofichua kuwa
yeye hula udongo kila siku kwa kupima kijiko kimoja.
Lakini je ni sawa kula udongo kwa sababu za kiafya?
Muigizaji huyo, aliyewahi kucheza
filamu mashuhuri ya Descendants akishirikiana na George Clooney, alisema
kuwa udongo ni moja ya vitu vyenye afya kwa mwili ambavyo yeye mwenyewe
anaweza kula.
![]() |
| Shailene Woodley |
nimegundua kuwa udongo unaweza kukupa afya nzuri mwilini. Najua wengi wanadhani kuwa mimi ni kichaa ninaposema kwamba , udongo una uwezo wa kusaidia kusafisha mwili wako kutokana na madini mazito mwilini
alisema Woodley.
Anasema alijifunza kula udongo kutoka kwa dereva
mmoja mwafrika. Baadhi ya marafiki zake hutengeza dawa ya kusugua meno
kutoka kwa udongo ambao unaweza kumeza. Hata hivyo alisema ni muhimu
kuwa udongo huo kabla ya kuliwa uwe safi.
Tabia ya kula mchanga au udongo inajulikana kwa kiingereza kama Geophagy.
Ni jambo la kawaida watu kula udongo Afrika au Mashariki ya kati
ingawa sharti uwe yametengezwa kwa mfano wa tembe. Hii ni kwa mujibu wa
mtaalamu wa afya katika hospitali ya Kings College, London, Rick Wilson.
Sababu muhimu ambayo inaweza kukufanya kula
udongo ni kukosa madini ya ZINC mwilini, lakini wataalamu wanasema
kukosa madini hayo mwilini sio hatari na kwamba sio jambo la kawaida
barani Afrika watu kukosa sana madini hayo mwilini.
Lakini Shailene Woodley anaamini kuwa kula udongo inaweza kukupa afya nzuri.
Udongo hata unaweza kuathiri mwili wako hasa ikiwa una chembechembe za Arsenic au Lead.
Wanawake wajawazito wakati mwingine hupata hamu
ya kula udongo au mkaa kwa kukosa madini fulani mwilini,anasema daktari
Sartah Jarvis.
Na inaweza kueleweka ikiwa ni barani Afrika kwa
sababu ya changamoto ya lishe bora lakini kula tu udongo kwa sababu ya
kupenda , hiyo haiwezekani.




0 comments:
Chapisha Maoni