STAA aliyewahi kutamba na songi la Presha, Hafsa Kazinja amesema anajuta
kuachika kwenye ndoa aliyokuwa ameolewa awali nje ya nchi na iwapo
atampata mume mwingine hatafanya makosa tena.
Hafsa alifunguka hayo
juzikati alipokuwa kwenye ‘Kitchen party’ ya mdada aliyetambulika kwa
jina la Nadhifa Ahmada iliyofanyika Sinza, jijini Dar.Mwenzenu najuta kuachika, nilifanya makosa lakini Mungu akinijaalia kwa sasa kupata mwanaume sitarudia makosa tena
alisema Hafsa pasipo
kufafanua kwa undani makosa aliyoyafanya.
0 comments:
Chapisha Maoni