Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa, iko katika mikakati ya kuhakikisha kwamba, inadhibiti hatua za wasichana kwenda China bila sababu maalumu ikiwa ni njia ya kudhibiti vitendo vya watoto wa kike kujihusisha na biashara ya ukahaba nchini humo.
Hatua hizo imechukuliwa kwa pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na Ubalozi wa China mjini Dar es Salaam.
Mkakati huo pia utashughulikia kuwarejesha nchini Tanzania washichana wa nchi hiyo walioko nchini China ambao imebainika kwamba, wanajihusisha na biashara ya ngono. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Mambo Nje ya Tanzania, Mkumbwa Ally katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Hivi karibuni Bernard Membe, Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema kuwa, mabinti wa Kitanzania wamekuwa wakifanyishwa biashara ya ukahaba huko China. Mji wa Guangzhou huko China ndio unaotajwa kwamba, wasichana wa Kitanzania wamekuwa wakifanyishwa biashara ya ukahaba.
0 comments:
Chapisha Maoni