Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ amepandishwa kortini kwa mara ya
kwanza huko Macau nchini China, Aprili 10, mwaka huu kwa kukutwa na
madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yakiwa na
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 huku ishu kubwa kwa muda wote
aliokuwa mahakamani ikiwa ni kuangua kilio kila wakati.
Jack alipandishwa kwenye korti hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu
alipokamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Desemba mwaka jana akitokea
Bongo kupitia Thailand na kuingia nchini humo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo Macau, Jack alifikia hatua
hiyo dakika 15 baada ya kupanda kizimbani na kukutana na nyuso za
Wachina tu zikimwangilia.
Yeye alijua angekuta Wabongo au hata watu weusi wakimpa kampani, lakini matokeo yake alikutana na sura za Wachina tu
kilisema chanzo
chetu.
Kikaendelea:
Unajua kwa kawaida mtu anapopanda kizimbani mara zote anafarijika sana endapo atawaona anaowafahamu, hasa ndugu zake ambao watafika kumtia moyo, sasa yeye hakulipata hilo
Kuna madai kwamba, msoma mashitaka wa mahakama hiyo alitumia dakika 10
kutokana na taratibu za kisheria za huko huku akitakiwa kusema ndiyo au
hapana tu kabla keshi hiyo kupigwa kalenda hadi Mei 23, mwaka huu.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kukutana na upweke
huo mahakamani, pia Jack alipata kisanga kingine pale baadhi ya raia wa
nchi hiyo walipomzomea kwa sauti ya chini wakati akitoka kortini.
Inadaiwa kuwa, kwa Wachina kumzomea au kumsema vibaya mtu aliyedakwa
na madawa ya kulevya ni kawaida kwani hakuna biashara, inapigwa vita
nchini humo kama ya unga wakiamini unaangamiza nguvu kazi ya kizazi
kijacho.
Habari nyingine kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, kwa sasa Jack amebaki yeye na Mungu wake baada ya nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima.
Habari nyingine kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, kwa sasa Jack amebaki yeye na Mungu wake baada ya nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima.
Unajua ndugu zake walikata mawasiliano kabisa? Nchi nzima au tuseme dunia nzima kilio ni jinsi vijana wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, sasa kule kubainika kwamba Jack alibeba unga tumboni kwenda kuuza kumeifanya familia kujisikia vibaya sana
kiliongeza chanzo hicho
kikiomba chondechonde kisitajwemtandaoni.
Habari zaidi zinadai kwamba modo huyo ambaye pia ni Miss Ilala No 3,
2005, aliwahi kumwambia mshirika wake mmoja akiwa mahabusu kwamba, kama
atabahatika kurejea Bongo salama,
atakwenda kupiga dua juu ya kaburi la mama yake ili amsimamie katika
kumwondolea nuksi kama siyo mabalaa. Baba wa Jack anadaiwa kuishi nje ya
nchi.
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka
jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akitokea jijini
Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la
Guangdong Kusini mwa China ambako ilidaiwa ndiko alikokuwa anafikisha
unga huo.
Ilidaiwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia kukamatwa kwake ni
kuonesha uso wenye uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa
kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria, yaani ‘passport’
kukutwa imegongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara jambo ambalo
wakaguzi waliliona si la kawaida kwa msichana kama yeye.
0 comments:
Chapisha Maoni