Jumatano, Aprili 09, 2014

MR BLUE AAHIDI KULIPA DENI KUBWA ANALODAIWA NA FANS WAKE MWEZI HUU

Mr Blue aka Kabayser ambaye kwa mwaka huu (2014) hajatoa wimbo mpya baada ya ‘Pesa’ iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana, amesema anatambua kuwa ana deni kubwa linalomuumiza kichwa analodaiwa na mashabiki wake na yuko tayari kulilipa siku si nyingi.
“Mwaka huu bwana nafanya video, inaniumiza kichwa kwasababu muda mrefu nadaiwa video na mashabiki”, alisema Kabayser leo.
Blue ambaye ana muda mrefu hajatoa video ya wimbo wake amesema anatarajia kufanya video ya ‘Pesa’ na atafanya na Adam Juma. “ndani ya mwezi huu (April) kwasababu nilishamalizana na Adam nasikilizia anipe tarehe niweze kupiga kazi”.
Baada ya video ya ‘Pesa’ kukamilika na kutoka mwezi ujao (May), Blue amesema atatoa wimbo wa crew yake ya Micharazo kabla ya kufikiria kutoa single yake mwenyewe mpya.

0 comments:

Chapisha Maoni