Meneja wa Arsenal,Arsene Wenger amethibitisha
kuwa Mesut Ozil atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu mpaka
sita kutokana na kupata majeraha ya misuli kwenye mchezo waliotoka sare
ya goli 1-1 dhidi ya Bayern Munich.
Kiungo huyo wa kijerumani alitolewa katika
kipindi cha kwanza Jumanne usiku kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya
16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya uliopigwa Allianz Arena na
tayari atakosa mchezo wa wapinzani wa Jiji dhidi ya Tottenham siku ya
Jumapili.
Mfaransa huyo alisisitiza kuwa,”Tumempoteza Ozil,ambaye amekuwa
majeruhi kwa kukosa mchezo wa Jumapili,Sifahamu atakuwa nje kwa kipindi
gani lakini inaweza kuchukua wiki kuanzia tatu.”
Na kuongeza,”Kama wastani ni wiki tatu basi inaweza kufikia wiki
sita.Sina uzoefu mkubwa wa kufahamu hilo zaidi ila ni tatizo la misuli
ya paja hivyo labda tuseme wiki nne.”
Kukosekana kwa Ozil kumekuja mara baada ya taarifa za Aaron Ramsey
kutokuwa fiti bado licha ya kuanza mazoezi pamoja na Jack Wilshere
ambaye naye bado anauguza majeraha ya kifundo cha mguu aliyopata kwenye
timu yake ya Taifa ya Uingereza.
Lakini kiungo mpya raia wa Sweden,Kim Kallstrom huenda akawepo White
Hate lane kucheza mchezo wake wa kwanza mara baada ya kusajiliwa kwa
mkopo huku akiwa majeruhi akitokea Spartak Moscow naye Nacho Monreal
anataraji kurejea.
Wenger aliongeza kuwa,”Ukweli ni pigo lakini najiamini tunaubora wa
kuweza kupambana bila Ozil.Tunawachezaji wengi hodari ambao wanaweza
kuchukua nafasi na kuonyesha kiwango kizuri.
0 comments:
Chapisha Maoni