Jumanne, Machi 11, 2014

WEMA SEPETU ALILIA MTOTO

Habari zilieleza kuwa Wema amekuwa na kiu ya mtoto kwa muda mrefu na kwamba alishakuwa na wanaume tofauti lakini hawakumpatia mtoto.
Ilisemekana kwamba katika msururu wa wanaume aliominya nao kimalavu, iliwahi kuripotiwa kuwa ni mwanaume mmoja tu aliyefanikiwa kumpa ujauzito lakini kwa bahati mbaya mimba ilichoropoka.
Mwanaume aliyekuwa na mzigo huo ilidaiwa ni Prezidaa wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.
Baada ya kupania kwa muda mrefu bila mafanikio, ilidaiwa kuwa mwanadada huyo mkali wa sinema za Kibongo aligeuzia mapenzi yake kwa mbwa (pets) wake wawili, Van na Gucc ambao mmoja wao amezaa hivi karibuni.
Habari zinadai kuwa, kutokana na mapenzi yake na mbwa hao, amekuwa akiwagharamia mkwanja mrefu katika chakula na shopping za mavazi ya bei mbaya.
WEMA ANAFAFANUA
“Nawapenda sana mbwa wangu, nawaona kama ndiyo watoto wangu kwani sina mtoto na ninatamani sana ila najua Mungu atanijalia siku moja muda ukifika,” alisema Wema na kuongeza:
“Kila jambo na wakati wake, nitapata tu, nadhani ni suala la muda tu. Watu wanaweza kushangaa namna ninavyowapenda mbwa wangu, nawathamini kwa sababu wananipa faraja na nipo nao karibu. Nawajali kama binadamu.”
Kabla ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayetoka naye kwa sasa, wengine waliowahi kuonja penzi lake na wakashindwa kumpatia mtoto ni pamoja na marehemu Steven Kanumba, Jumbe Yusuf na Chaz Baba.

0 comments:

Chapisha Maoni