Jumatatu, Machi 24, 2014

WATU 529 WAHUKUMIWA KIFO

Mahakama nchini Misri imewahukumu kifo watu 529 ambao wanasemekana kuwa wafuasi wa Rais aliyeng'olewa mamlakani Mohammed Morsi.Watu hao walikabiliwa ma mashitika mbali mbali yakiwemo mauaji ya polisi na kuwavamia polisi.
Wafuasi hao wa chama kilichopigwa marufuku, cha Muslim Brotherhood, ni sehemu ya kundi lengine kubwa la watu zaidi ya 1,200 wanaoaminika kuwa wafuasi wa Morsi.Maafisa wa utawala nchini Misri wamekuwa wakiendesha msako mkubwa dhidi ya wafuasi wa vuguvugu hilo, tangu Morsi kuondolewa mamlakani mwezi Julai mwaka jana.
Maelfu wamekamatwa huku mamia wakiuawa.Mahakama hiyo ilitoa hukumu baada ya vikao viwili pekee ambapo mawakili wa watuhumiwa walilalamika kuwa hawakupewa muda wa kuwasilisha kesi yao vyema.
Mauaji wanayodaiwa kufanywa na watuhumiwa yalitokea Kusini mwa Misri, mwezi Agosti, baada ya vikosi vya usalama kuvunja kambi mbili za wafuasi wa Morsi waliokuwa wanataka arejeshwe mamlakani.

0 comments:

Chapisha Maoni