NDEGE ya abiria ya Malaysia iliyopotea kiutatanishi
wiki mbili zilizopita, inadaiwa iliruka chini ya futi 12,000 kutoka
usawa wa bahari kutokana na matatizo katika chumba cha rubani kabla ya
kupotea katika rada, ripoti mpya zimeeleza.
Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia, Warren Truss, kulia, akizungumza na ofisa wa juu wa kikosi cha uokoaji na mratibu wa operesheni ya kuitafuta ndege iliyopotea, John Rice. |
Wakati ndege hiyo Boeing 777-200 ikiwa bado inatafutwa katika Bahari
ya Hindi, habari zinasema chombo hicho kilibadili uelekeo kikiwa juu ya
bahari ya Kusini ya China.
Wataalamu wa rada wakiwa ndani ya ndege ya Kijeshi ya New Zealand katika msako wa chombo hicho kilichopotea kusini mwa Bahari ya Hindi. |
Mara ya mwisho ndege hiyo ilionekana katika rada ya Jeshi la Malaysia
saa 2.15 asubuhi kwa saa za nchi hiyo, Machi 7 mwaka huu, ikiwa katika
kisiwa cha Penang kilicho kusini mashariki mwa taifa hilo, muda kama saa
moja baada ya kuwa imeruka kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing nchini
China.
Naibu Waziri Mkuu wa Australia Warren Truss akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya utafutwaji wa ndege iliyopotea. |
Mapitio ya rada yalionyesha ndege hiyo ikibadili mwelekeo baada ya
kugeuka ghafla na kwa kasi upande wake wa kushoto kuelekea Malacca.
Mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha maji cha China akiendelea na msako wa ndege iliyopotea kusini mwa Bahari ya Hindi. |
Mike Barton, mkuu wa kikosi cha uakoaji, kushoto, akiangalia ramani ya Bahari ya Hindi akiwa na Alan Lloyd, ofisa wa kitengo cha uokoaji katika Jeshi la Majini Australia. |
Ofisa mmoja aliyekataa kutajwa jina kwa vile siyo msemaji, aliiambia
CNN kwamba kuruka chini ya futi 12,000 katika anga yenye ndege nyingi
kama ilipokuwa ikipita kungeifanya ndege hiyo kutoonekana na ndege
zingine.
0 comments:
Chapisha Maoni