Ijumaa, Machi 07, 2014

UTHIBITISHO ZAIDI KUWA SOLO THANG AMEZAA MTOTO NA WASTARA JUMA JAPO ILIFANYWA SIRI KUBWA

Kumbe staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma, aliye mama wa watoto watatu, mmoja kati yao, alizaa na mkongwe katika Bongo Hip Hop, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika kilipasha kuwa Wastara amekaa na siri hiyo moyoni kwa muda mrefu sana.
“Mtoto mmoja alizaa na Solo, wakati ule Solo akiwa anatamba na nyimbo zake kama Homa ya Dunia, Mambo ya Pwani na Mtazamo ambao alishirikiana na Afande Sele na Profesa Jay. Tena leo (juzi Jumatano) ameandika kwenye Instagram na ameweka na picha ya Solo,” alipasha shosti huyo.
Haraka paparazi wetu, akazama kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kufanikiwa kuona picha hiyo iliyosindikizwa na maneno: “Baba wa baby wa miye, Msafiri Kondo a.k.a Solo Thang, moyo wako haukupishana sana na wa Sajuki (Juma Kilowoko).
“Sijawahi kuyasema haya lakini utazipata salamu huko ulipo. Maisha yametutenganisha ila sijawahi kugombana na wewe wala familia yako. Nashukuru kwa upendo wenu juu yangu hasa mama yako. Nawapenda sana na hata mtoto wenu anawapenda. Dunia ni njia tu, hatujui nani atatangulia. Nakutakia mafanikio. Inshallah.”
Baada ya kupandiwa hewani Wastara ili kupata ufafanuzi juu ya ishu hiyo ambapo alikuja juu: “Hivi kwa nini mnanifuatafuata sana jamani? Sasa umesema umeona Instagram, kwa hiyo nikusaidie nini?”

0 comments:

Chapisha Maoni