Ijumaa, Machi 07, 2014

HIZI NDIO SABABU KUBWA ZINAZOWEZA KUMFANYA MWANAMKE ASIFURAHIE TENDO LA NDOA

Ni wanawake wachache sana wanaofikia climax pia si wanawake wote wanaenjoy sex, sasa ulishajiuliza kwanini hauenjoy?? Kwa utafiti wangu kuna vitu nimegundua ndo mara nyingi hupelekea mwanamke asifurahie tendo hilo au asiridhike

1. Kama hajampenda mwenza wake, ni vigumu kufurahia tendo hili kama huyo unaefanya nae hujampenda au hata kumfeel kidogo. Kama mapenzi kwa mchumba wako yameisha usifikiri ukifanya nae mapenzi utafurahi, unajidanganya!! hakuna kitu hapo labda aridhike yeye tu.


2. Kufanya mapenzi kwa malengo fulani, hata siku moja huezi kufurahia sex huku ukiwa na nia ya kufaidika na kitu fulani kutokana na hilo tendo kwasababu najua muda wote utakuwa unatamani huyo mwanaume amalize saa ngapi ili upate unachokitaka na hii inatokea kwa wasichana wanaojiuza(machangudoa) na pia hata kwa wale wenye mahusiano na vizito na mapedeshee anafanya sex huku akijua atafaidika na nini na mara nyingi hawa wanakuwa hawana mwanaume mmoja

3. Mawazo, unafanya sex ukiwa na msongo wa mawazo. Hauwezi kuenjoy huku unawaza mtoto anaumwa au tatizo lolote tu linalokukabili pia kwa wanawake wenye mwanaume zaidi ya mmoja wanakuwa na hofu za kufumaniwa so akili yake haitakuwepo hapo kabisa na hivyo kusababisha upande mmoja tu kufurahia tendo

4. Kutoandaliwa, hili ni kosa ambalo wanaume wengi wanafanya, mwanamke ni lazima aandaliwe ili naye afurahi. Mwili wa mwanamke unahitaji taarifa kuweza kujua kitu gani kinakuja ili kuweza kulainisha viungo vya mwanamke na asiweze kuchubuka wakati wa tendo jua kwamba mwanamke akiwa mkavu lazima ataumia na hatoweza kufurahia tendo. ILA katika mzunguko wa mwanamke kuna siku ambazo sehemu zake nyeti huwa kavu sana hata kama mwanamke atakuwa na hamu sana, sasa ukiona hali hii ni vizuri mkatumia vilainishaji au mafuta maalum

5. Ugonjwa, kuna baadhi ya magonjwa humfanya mwanamke asiwe na hamu kabisa na sex hapa ningependa kuwaachia madaktari zaidi, kama unajua huna tatizo lolote kati ya niliyoyataja hapo juu basi nenda kamuone daktari utakuwa unatatizo linngine, na hii pia hutokea nilishashuhudia rafiki yangu akiwa na hili tatizo kumbe alikuwa na tatizo dogo tu ambapo alitibiwa akapona sasa yuko freeeeeesh!

0 comments:

Chapisha Maoni