Alhamisi, Machi 20, 2014

UKITAKA USALAMA KWENYE MAPENZI USIFANYE MAKOSA HAYA.

Zipo alama muhimu ambazo ni vema kuzijua na uzibaini kwa mwenzi wako kabla hujazama kwenye dimbwi la mapenzi. Bahati mbaya wengi hutawaliwa na papara, matokeo yake hushindwa kubaini vitu ambavyo vinaweza kumfanya apate uelekeo wa uhusiano wake.
Mantiki hapa ni kukutaka uwe makini na umsome mwenzako kwa undani kabisa. Katika kipengele cha kusoma alama muhimu, kuna vitu vya msingi vya kuzingatia ambavyo ni hivi vifuatavyo;
 
1. JAMII: Mwenzi wako anasimama vipi na jamii yake? Usiingie kichwa kichwa kwenye mapenzi na mtu ambaye hata jamii yake inamuona ni tatizo. Vilevile, yule ambaye ni muoga inabidi uanze kumtia wasiwasi mapema. Ni kwa ajili ya maisha yako, hivyo ni vema kuchangamka.
Hutakiwi kugundua muda umeshapita kuwa mwenzi ana tabia usizopenda. Mapema msome na umuelewe. Chunguza msimamo wake kwenye jamii, anavyojiamini, je, anaonesha kuwa na dira ya maisha. Kama hana uelekeo, unatakiwa kuachana nae mara moja msije mkapoteza muelekeo pamoja bure.
2. HISIA: Zisome hisia zake, je ni mtu anayejali? Unatakiwa kujua kama hisia zake zipo karibu kwa kiasi gani. Atakapotakiwa kukutimizia haki yako ya faragha, atakuwa tayari kwa wakati?
Ni aibu mmeshakuwa na uhusiano kwa muda mrefu ndiyo unaanza kulalamika kwamba mwenzi wako hakutimizii huduma ya uwanja wa wawili.
3. MUONEKANO WAKE: Ni kipengele kidogo muhimu ndani ya kifungu cha kushindwa kusoma alama kama sehemu moja wapo inayowafanya wengi kufanya makosa kwenye uhusiano.
Muonekano si suala la baadaye, inatakiwa mapema sana umtathmini halafu ujiridhishe kama anakufaa au kinyume chake.
Ni aibu umeshaingia kwenye uhusiano, halafu baadaye unamsaliti mwenzi wako na kuanza kuwatolea macho wale ambao unaona ni wazuri zaidi.
Hakikisha kwamba mwanzo kabisa kwenye uhusiano wako, unajiridhisha kuwa anao mvuto unaokutosha.

0 comments:

Chapisha Maoni