Alhamisi, Machi 20, 2014

KENYA YATOA DARASA KWA BUNGE LA KATIBA TZ

Ujumbe maalum kutoka nchini Kenya umehutubia wajumbe wa Bunge la Katiba nchini Tanzania kuelezea uzoefu wao kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya nchini Kenya ulivyofanyika.
Akizungumza na Wajumbe wa Bunge maalum la katiba, Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Kenya,
Amos Wako ameainisha masuala ya msingi ya kuzingatia katika upatikanaji wa Katiba mpya ya Tanzania.

Bwana Wako ameeleza uzoefu wake wa upatikanaji wa katiba ikizingatiwa kuwa wakati mchakato wa kupata katiba mpya nchini Kenya alikuwa miongoni mwa watendaji wakuuu wa mchakato huo akiwa mwanasheria mkuu wa serikali.
Bwana Wako amewataka wajumbe wa bunge maalum la katiba nchini Tanzania kuzingatia historia, utamaduni na matakwa ya watanzania.
Wako amesema kuwa baada ya machafuko ya nchini Kenya na jumuia ya kimataifa kuingilia kati, mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya usuluhishi iliyoongozwa na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan yaliona kuwa suala la kupata Katiba mpya nchini Kenya, lichukuliwe kuwa suala la Haraka na dharura.
Semina hii kwa Wajumbe wa Bunge la katiba imekuja wakati Rais wa Tanzania Jakaya kikwete akitarajiwa kufungua rasmi Bunge maalum la Katiba siku ya Ijumaa mjini Dodoma katikati mwa Tanzania

0 comments:

Chapisha Maoni