Jumatano, Machi 26, 2014

SUDAN KUSINI YATAHADHARISHWA

Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kwamba mamilioni ya watu wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula huko Sudan Kusini, huku msimu wa mvua ukikaribia nchini humo.
John Ging Mkurugenzi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA) amesema kuwa, kuna uwezekano wa kutokea janga kubwa la ukosefu wa chakula katika nchi hiyo iliyokumbwa na machafuko hivi karibuni. Ging ameongeza kwamba, watu milioni 5 wanahitajia misaada ya dharura na mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa imeshindwa kutayarisha misaada ya chakula kabla ya kuanza msimu wa mvua.
Zaidi ya watu laki 7 wamelazimika kukimbia makazi yao nchini Sudan Kusini tangu mwezi Disemba yalipoanza machafuko kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji watiifu kwa makamu wa zamani wa Rais Riek Machar.

0 comments:

Chapisha Maoni