Jumapili, Machi 30, 2014

STAA WA BONGO FLEVA AKANA KUTOA PENZI KWA MAMENEJA

STAA wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda amewachana wasanii ‘wanaotembea’ na mameneja wao kwani ni ujinga wa mawazo na yeye kamwe hawezi kufanya hivyo.
Akizungumza na mtandao huu hili, Isabela alisema katika maisha yake hajawahi kuwa na uhusiano na meneja au prodyuza na huwa anawashangaa na kuwasikitikia wasanii wanaofanya hivyo wakati siyo njia sahihi ya kujikwamua kimuziki.
“Huwezi kuchanganya kazi na mapenzi, kamwe siwezi kutoka kimapenzi na meneja wangu kwa sababu najua ufanisi wa kazi utakuwa mdogo tu,” alisema Isabela.

0 comments:

Chapisha Maoni