Jumapili, Machi 30, 2014

MTOTO WA MIAKA TISA ASHIRIKI NGONO NA WATU WAZIMA, BIBI AOMBA MSAADA

Mpaka sasa mtoto huyo ana miaka tisa, lakini mchezo huo umekuwa sehemu ya maisha yake na kuathiri hata uwezo wake darasani. Endelea kujua kilichofuata.
Baada ya kukagua daftari za mtoto huyo na kuona hesabu ambazo haziendani na mwanafunzi wa darasa la pili, bibi Lebai alilazimika kwenda shule kwa lengo la kuzungumza na walimu kujua inakuwaje.
Anasema alipofika shuleni na kukutana na mwalimu wa mtoto huyo akagundua kuwa hesabu hizo hazikuwa zikifundishwa darasani wala kusahihishwa na mwalimu kama alivyokuwa akidhani.
Anaeleza kuwa baada ya kuona daftari kwa haraka mwalimu akagundua mwandiko huo ulikuwa wa mwanafunzi wa kiume wa darasa la nne ambaye alimtaja kwa jina.
“Mwalimu alivyoangalia tu akasema huu ni muandiko wa kijana fulani wa darasa la nne, nadhani alikuwa anamuandikia na kumsahihishia muda wanaokutana na alikuwa anafanya hivyo ili nisipate la kumuuliza maana alikuwa akipata hesabu zote,” anasema.
Jambo hilo lilimkwaza na kuona kuwa mtoto huyo hawezi kubadilika akiwa shuleni hapo, akalazimika kumhamishia kwa shangazi yake ambako alihisi huenda mazingira mapya yangembadilisha tabia.
Anasema akafanya taratibu zote na kumhamishia katika shule ya msingi Kunguru iliyopo Tegeta Mbuyuni, lakini huko ndiko hali ilipozidi kuwa mbaya zaidi kwani alikuwa akitumia muda mrefu kushinda porini kufanya mchezo huo na wanafunzi wenzake.
“Nikajua kule atakuwa mgeni huenda ndiyo ingekuwa mwisho wa mchezo wake kumbe kule ndiyo ilikuwa balaa kuna pori moja ambalo ndiyo limekuwa sehemu yake anawachukua wanafunzi wenzie na kwenda nao huko,” anasema na kuongeza:
“Nikaanza kupata malalamiko kutoka kwa shangazi yake kuwa anachelewa mno kurudi, na hata akirudi anakuwa amechafuka kiasi kwamba ni ngumu kuamini kuwa alikuwa shuleni”.
Anasema akajaribu kuanza tena kumchunguza mwenendo wake na kugundua kuwa huwa haandiki, na hata anapoandika daftari zake hazisahishwi na walimu.
“Mwenendo wake wa kuchelewa kurudi ulinifanya nianze tena kumchunguza kwa undani nikawa naangalia daftari zake, nikaona ameanza uvivu wake wa kutoandika na kusahishiwa daftari nikalazimika kwenda tena shuleni kujua maendeleo yake,” anasema.
Anasema alipofika na kujitambulisha kwamba ni bibi wa mtoto huyo walimu walimshangaa na kumuelezea kuwa hawakuwa wakiuelewa mwenendo wake kutokana na muonekano wake kuhisi kuwa huenda ana matatizo ya akili.
“Walimu wake walinishangaa wakaniambia kila siku wanamwambia amlete mzazi wake ila akawa anawazungusha, wakasema pia kuwa shule huwa anafika lakini haandiki,” anasema.
Walimu wakambana ili aseme mahali anaposhinda muda ambao wenzake wanakuwa darasani, bakora alizochapwa na mwalimu wake zilimsukuma kuwataja wote ambao waliwahi kumuingilia.
Anasema alitaja orodha ndefu ya watu ambao wamewahi kumuingilia kimwili wakiwamo wanafunzi wenzake pamoja na vijana wengine ambao wanaonekana kuwa na umri unaokadiriwa kufikia miaka 30.
“Akaandika majina hayo mwenyewe kwenye karatasi, binafsi nikaona ili kumuepusha na dhahama hiyo ni bora akae nyumbani asiende shule maana huo ndiyo upenyo anaoutumia kufanya mchezo wake.
“Lakini kila ninapofikiria umuhimu wa elimu naona nitamkosesha huyu mtoto kupata haki yake ya msingi, ndiyo maana naomba msaada aweze kupata shule ya bweni ya wasichana tupu ambayo pia itakuwa na misingi ya dini huenda akabadilika na kuwa kama watoto wengine,” anasema.
Anasema pamoja na suala la shule huenda mtoto huyu anahitaji matibabu kwa kuwa tabia hiyo inaonekana kuathiri akili yake kiasi kwamba hata muda anaokuwa mwenyewe anadiriki kuchana nguo zake za ndani.
“Ukiangali nguo zake za ndani karibu zote katikati zina matobo anatoboa ili awe anajiingiza vidole,wakati mwingine hata akilala na watoto wenzake wanalalamika anapenda kuwapapasa kitu ambacho nahisi hata kwenye akili yake hatakuwa sawa,” anasema.
Baada ya kupata maelezo hayo ya bibi Lebai, mwandishi wa makala haya alifanya jitihada za kumpeleka mtoto huyo hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kujua hali yake ya afya kwa ujumla.
Vipimo vilichukuliwa na Dk. Rose Mbeyele wa Hospitali ya Rufaa ya Amana ambaye alithibitisha mtoto huyo kuingiliwa kimwili sehemu zake za siri mbele na nyuma.
Jambo la kushukuru majibu ya damu na mkojo hayakuonyesha mtoto huyo kuwa na tatizo lolote kiafya wala dalili za kunyemelewa na ugonjwa wowote wa zinaa kwa wakati huo.
Hata hivyo mwandishi wa makala alifanya jitihada za kumtafuta mama wa mtoto huyo, kujua sababu ya kuruhusu mtoto wake afanyiwe ukatili wa aina hii tena angali akiwa mdogo mpaka sasa tatizo linazidi kuwa sugu.
Mwanamke huyo anayejitambulisha Julieth Anthony anasema ugumu wa maisha ulimfanya kushindwa kuishi na watoto wake wawili, hivyo kushindwa kushiriki kikamilifu katika malezi.
Anasema tangu amzae mtoto huyu hajapata fursa ya kukaa naye kwa muda mrefu ili kujua tabia na mwenendo wake wa kila siku na hilo linasababishwa na ugumu wa maisha, kutokana na kukosa shughuli maalumu ya kufanya.
Hata hivyo Julieth anakiri kuwa mtoto wake alianza kuharibika wakati yuko naye kutokana na mihangaiko aliyokuwa nayo, hali iliyokuwa ikimsababishia mara kwa mara kumuacha mtoto huyo peke yake.
“Katika harakati za kujitafutia riziki nilikuwa naamka asubuhi na kwenda kuuza chapati mbali kidogo na nyumbani nikiwa nimemuacha mtoto kumbe wakati huo ndiyo alikuwa akifanyiwa mchezo huo na mtoto wa mpangaji mwenzangu.
“Bibi yake alipokuja kumchukua ndiye aliyemhoji na kujua hilo kiukweli kama mama niliumia lakini sikuwa na namna ya kufanya, kwa sasa binafsi sijui kama anaendelea au ameacha kwa kuwa sijapata fursa ya kuishi naye tangu alipochukuliwa akiwa na miaka miwili,” anasema.
Kuhusiana na kushindwa kutimiza wajibu wake kama mama kwa mtoto huyo anasema hilo lilitokana na kutengana na baba wa mtoto huyo baada ya kuzaliwa hali iliyomsababishia watoto wake wawili kulelewa na bibi yao.
Anasema kwa muda mefu kumekuwa na hali ya kutoelewana kati yake na ndugu wa mzazi mwenzake akiwamo bibi anayemlea mtoto huyo hivyo kushindwa kabisa kujua maendeleo yake.
“Sina kazi wala biashara maisha yangu ni ya kubaingiza vilevile sina maelewano mazuri na mama mkwe wangu, hali inayosababisha mimi kushindwa kumlea mwanangu na matokea yake anajihusisha kwenye tabia za ajabu napatwa na uchungu sana kama mama, lakini sina cha kufanya hiyo yote kwa sababu ya umaskini,” anasema.

1 comments:

  1. Nipeni huyo mtoto mimi.Sidhani kama an shida kubwa kiasi hicho. Hakuna kinaweza kushindikana. Atafika mbali sana kimasomo. Niko Moshi.

    JibuFuta