Msanii nguli katika filamu za Bongo. Shamsa Ford amenusurika kifo baada ya gari lake kugongana na lingine.
Akichonga na paparazi wetu, Shamsa alisema tukio hilo lilitokea
juzikati maeneo ya Sayansi akiwa na gari aina ya Noah aliligonga gari
aina ya Vitz na magari yote yakaharibika vibaya lakini bahati nzuri
hawakuumia.
“Kweli ni Mungu tu maana ajali ilikuwa mbaya, nashukuru sijaumia ila
gari langu ndilo limeharibika vibaya, ilibidi nilifanye ustarabu
nikatengeneza magari yote,” alisema Shamsa.
0 comments:
Chapisha Maoni