Mwanafunzi wa shule ya Makongo, Priscus Mallya amegongwa na lori na kufariki papo hapo. |
Ajali mbaya imetokea hivi punde katika barabara ya Bagamoyo iyendayo
Mwenge ambapo mwanafunzi mmoja wa shule ya Makongo (jina bado
halijapatikana) amegongwa na lori na kufariki papo hapo.
Kwa mujibu wa watu waliowahi tukio hilo likitokea, wanasema kuwa
mwanfunzi huyo alikuwa ndani ya bajaji akielekea shuleni Makongo ambapo
walikutana uso kwa uso na lori kisha kumrusha na kutokea upande wa pili.
Dereva wa bajaji yupo, lori limetokomea na mpaka tunaingia mtamboni
tayari baadhi ya bodaboda zipo katika jitihada za kulifuatilia lori
lilipoe lekea.
0 comments:
Chapisha Maoni