Jumatatu, Machi 24, 2014

PICHA HIZI CHAFU ZA HUDDAH ZAMFANYA NYOTA NDOGO NA WANAWAKE WENGINE NCHINI KENYA KUANDAMANA, ZIPO VIDEO MBILI PIA

Colonel Mustapha ni miongoni mwa Wasanii wa longtime kidogo kwenye game ya muziki Kenya toka enzi hizo akiwa kwenye kundi lililotoa hit single yenye maneno ‘bibi yake mufupi, kijana murefu ametoka wapi’
Hivi karibuni ameingia kwenye vichwa vya habari sana hasa baada ya kutangaza kuwa mapenzini na Huddah, mrembo aliewahi kuiwakilisha Kenya kwenye shindano la Big brother Africa ambapo uhusiano wao hauchukua muda mrefu ukavunjika.
Kabla ya kuvunjika, tayari walikua wameshapiga picha ambapo Mustapha anasema alikua amerekodi wimbo na Huddah lakini walipoachana mrembo huyu akasema Ogopa Dj’s wasiitumie tena sauti yake kwenye huo wimbo na kama watafanya hivyo atawashitaki.
Hata hivyo picha zao wawili zilishasambaa kwenye internet tayari na kuanza kuchukua headlines kutokana na pozi zao.
Kuonyesha kupinga hiki kitendo, mwimbaji staa wa ‘watu na viatu’ Nyota ndogo aliungana na Wanawake wengine Mombasa na kuandamana kupinga kitendo cha Mustapha kuzisambaza picha zinazomdhalilisha Mwanamke hivyo aombe msamaha haraka iwezekanavyo.
Hata hivyo Mustapha amezungumza baada ya haya maandamano na kusema ‘Ni kitu cha kushtua kuona maandamano yamefanyika kwa ajili ya Mustapha, wakati tunapiga hizi picha hakukua na lengo lolote la kumdhalilisha Mwanamke bali ilikua mambo yetu yenyewe kwa raha zetu, nilivyoona youtube kuhusu haya maandamano nimehuzunika… naomba msamaha kwa yeyote aliekerwa na hili… nimekubali kuomba msamaha kwa Wanawake’
Kwa kumalizia Mustapha amesema ‘kuna Wasichana ambao wanataka tupige hizo picha na wananilipa’ 

0 comments:

Chapisha Maoni