KUCHAMBANA, kutoleana lugha chafu ndiyo ishu iliyopo kwa sasa kati ya
nyota wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper na mshiriki wa Miss Tanzania
mwaka 2011 iliyomtoa mlimbwende Salha Israel, Husna Maulid kufuatia
madai kwamba, wanamgombea mwanamume Mkongo aliyejulikana kwa jina moja
la Mwami.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Husna ndiye aliyeanza kuwa na uhusiano na
Mkongo huyo mwaka jana na kila anapofika nchini hutanua naye kwenye
‘viwanja’ mbalimbali.
“Husna ndiye mwenye mwanaume, akija Bongo wako wote, lakini hivi
karibuni ghafla tu, jamaa kaja na kuwa na Wolper, Husna kapigwa chini,
sijui Wolper alimpatia wapi?” kilisema chanzo hicho.
Jumamosi iliyopita, Uwazi lilimtafuta Husna na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alifunguka kwa kusema:
“Ni kweli kabisa, Wolper amenichukulia mwanaume wangu. Mi nimemshangaa sana. Halafu eti ananitumia meseji za ajabu ajabu mimi, eti anasema hajanichukulia b
“Ni kweli kabisa, Wolper amenichukulia mwanaume wangu. Mi nimemshangaa sana. Halafu eti ananitumia meseji za ajabu ajabu mimi, eti anasema hajanichukulia b
ali ni bwana ‘ake siku nyingi (huku akionesha meseji hizo).
Baadhi ya meseji hizo zinaonesha Husna akijibu mapigo upande wa pili
huku akishambulia kwa maneno makali kufuatia madai kwamba anatembea na
Mkongo wake.
“Jana (Ijumaa) alikwenda naye hoteli…(anaitaja jina) iliyopo Masaki
(Dar), wakala chakula kisha wakaenda kulala hoteli… (pia anaitaja jina).
Mimi najua kila kitu,” alisema Husna akionesha hasira.
Kwa mujibu wa Husna, awali siku hiyo alitaka kwenda kumfumania Wolper na Mkongo huyo kwenye hoteli waliyokuwa wakila chakula lakini machale kama yalimcheza wakaondoka.
Kwa mujibu wa Husna, awali siku hiyo alitaka kwenda kumfumania Wolper na Mkongo huyo kwenye hoteli waliyokuwa wakila chakula lakini machale kama yalimcheza wakaondoka.
Baada ya kuzungumza ana kwa ana na Husna, Uwazi lilimsaka Wolper kwa
njia ya simu ili kumuuliza lakini hakupokea. Wakati mwingine simu yake
ilipopigwa ilionekana kuwa bize.
Hata hivyo, ili kumpa nafasi zaidi ya kujieleza, Wolper alitumiwa
meseji saa 5:05 asubuhi ikiwa na mashitaka yote ambapo ‘ilideliva’
kwenye simu yake, lakini pia hakuijibu mpaka saa 10:13 jioni wakati
gazeti hili linakwenda mitamboni.
0 comments:
Chapisha Maoni