Alhamisi, Machi 27, 2014

NYOTA YAKO LEO IJUMAA: 28/3/2014

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo inaonekana una furaha na hupendi mtu yoyote akukasirishe, lakini jiepushe sana na marafiki au washirika ambao unaona watakukasirisha. Inaonekana hao marafiki wanadhamira ya kukuudhi. Tafuta sababu yoyote ya kuwakwepa.
NG’OMBE –TAURUS (APR 21 – MAY 20)
Umefanikiwa kujiepusha na kufanya maamuzi mazito sana katika kipindi cha mwezi mzima uliopita. Inaonekana kabisa kwamba ndani ya moyo wako unajua kabisa kitu gani cha kufanya na ukifanye lini lakini unashindwa kufanya kwa sababu unataka kumhifadhi mtu./ Mwezi huu amua moja.
MAPACHA – GEMIN (MAY 21 – JUN 21
Kuna jambo la kukufurahisha limekutokea kazini na limekufanya uache mambo yote ili kulishughulikia. Kama utajisikia umechoka kiakili fanya mazoezi au kimbia au tembea tembea. Kuna uwekezakano wa kukutana na rafiki au mshirika wako ambaye atakufanya ufurahie maisha wiki hii.
KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 22
Leo inaonekana kuwa alkhamisi itakayokuwa na matatizo kwako, jitahidi kufanya machache utakayoweza ili kuepukana na matatizo. Jiahidi wewe mwenyewe kwamba utatekeleza majukumu yaliyobaki wiki ijayo. Uwezekano wa kutekeleza upo unachotakiwa kufanya ni kutumia akili na ujasiri.
SIMBA – LEO (JUL 23 – AUG 22)
Inaonekana ni siku ya mapenzi na mahaba kwa sababu sayari ya mwezi inaingia katika nyota yako.Hii vile vile inaonyesha kwamba mazingira yatakuwa tofauti na unavyofikiria hivyo kuwa muangalifu sana na watu usiowafahamu.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Kama mpenzi wako anakulalamikia kwamba hakupati vile inavyotakiwa kubaliana nao kwa sababu wanasema ukweli.Sayari ya Zohal imesimama katika nyota yako na ndio inakufanya usiwe na muda kushughulikia masuala ya mapenzi. Wafanye uwapendao wajue jinsi unavyoshughulika, hiyo ndio njia ya kuwa nao karibu.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo unaonekana una mambo mengi yanayokushughulisha kama ilivyokuwa wiki iliyopita na shughuli za kazi zimeongezeka kidogo. Fikiria sana Je hizi kazi kuna mtu anakujazia uzifanye au unazifanya kwa ajili ya kuinua hadhi yako? Kama ni la kwanza tafuta sababu ya kukwepa kama ni la pili jipunguzie majukumu utaumia.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Hii ni siku nzuri kama ukiwa na mpango wa kununua Nyumba au gari au kitu chochote. Manunuzi yote makubwa yana baraka zote ukiwa wewe mwenyewe au ukiwa na mshirika wako. Kama unafanya kazi Benki au katika kampuni ya Bima huo ndio wakati hasa wa kufanya mipango yako ya kimaisha.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Leo fanya mawasiliano na jamaa zako walio nje ya nchi. Kama kazi zako zikiwa zinahusiana na wageni utapata nafasi nzuri itakayokushangaza. Kama una mpenzi anaishi nje, basi tegemea kupata habari za kufurahisha za mualiko wa kumtembelea.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo Sayari ya jua inaingia katika nyota yako na hiyo inashiria kuanza kufunguka kwa mambo yako yaliyokwama, utapata marafiki wengi wa jinsia tofauti na yako ambao watakuburudisha na kukufurahisha. Ni wakati mzuri wa kufanya starehe.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Je unatafuta mpenzi? Sayari zote zinazohusiana na mambo ya mapenzi ziko kwenye nyota yako wiki hii. Utapata wapenzi wapya, waliotoroka watarudi, waliowakorofi wataacha ukorofi wao na waliokukatalia watakubali. Tumia wakati huu kujifurahisha.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
siku nzuri na ya bahati kwako ukishindwa kutumia bahati hiyo usijilaumu, wala usiseme umetengwa. Toka tafuta nafasi, fanya uhusiano, waendee wenye pesa wakukopeshe, fanya biashara, anza kujenga, nunua nyumba na chochote. Changamka usilale

0 comments:

Chapisha Maoni