MSANII wa filamu za Kibongo, Abdulmalick Ahmed
‘Ben’ anasakwa na jeshi la polisi akidaiwa kumjeruhi mzazi mwenziye,
Leyla Abdalah, mkazi wa Magomeni-Mikumi, Dar.
Akizungumzia tukio hilo, Leyla alisema mwigizaji huyo ambaye pia
hufahamika kwa jina la Serengo amekuwa akimfanyia fujo mara kwa mara
kwani Januari, mwaka huu, akiwa katika Ukumbi wa Travertine, Magomeni,
Dar, alikutana na msanii huyo ambaye alimlazimisha waondoke pamoja,
alipokataa akaanzisha vurugu.
Leyla alisema kwa kuwa msanii huyo walishamwagana kwa talaka tatu
miaka mitatu iliyopita, alikataa kuondoka na mzazi mwenziye huyo na
kudai mbali na kuachana naye, alikuwa na mpenzi wake mpya.
“Nilimuambia siwezi kwenda naye popote, alinivamia na kuanza
kunishushia kipigo kikali na kunichania nguo mbele za watu, wadau
walijaribu kugombelezea sikujisikia poa ndipo nikakimbizwa Hopitali ya
Magomeni, Dar nikalazwa wodi ya mapumziko, nikatoka,” alisema Leyla na
kuongeza:
“Nikiwa katika maumivu ya kipigo hicho, Jumamosi iliyopita Ben
alinishushia tena kipigo cha mbwa mwizi baada ya kukutana naye kwenye
Baa ya Kilimanjaro, Magomeni-Mapipa.
“Anilikuta na wenzangu, akanivamia tena na kuniambia anataka
tuondoke, nilipomuuliza twende wapi, akanijibu kwa ukali weee twende tu,
nikamkatalia, akapanda juu ya meza na kunijeruhi kichwani na kiti ndipo
nikaona bora nikimbilie Kituo cha Polisi cha Magomeni.
“Nilimfungulia kesi kwenye jalada lenye namba MG/RB/1234/14 SHAMBULIO
LA KUDHURU MWILI,” alisema Leyla. Baada ya
Ben nakumsomea madai ya mzazi mwenzake huyo ambapo alikiri kuzaa naye na kudai migogoro hiyo inasababishwa na yeye kudai mtoto wake.
“Huyo mwanamke ni kweli nilizaa naye lakini kwa sasa sina haja naye
hata kiduchu, nina mwanamke yuko bomba ile kinoma ukimuona mwenyewe
utabloo, siwezi kurudia matapishi.
“Huyo anataka kuniharibia tu, kila nikimfuata anipe mtoto wangu
anajifanya mpana na kuniletea ndivyo sivyo ndiyo maana tunakwaruzana
mara kwa mara,” alisema Ben.
0 comments:
Chapisha Maoni