Tanzania ilishindwa kujadiliana na Malawi kuhusu mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kwa miaka mingi kutokana na kipindi hicho kuwa katika harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, huku Taifa hilo (Malawi) likiwakumbatia makaburu wa Afrika Kusini na hivyo kuwa katika mazingira ya uadui.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Membe alisema hiyo ni miongoni mwa majibu ya hoja kadhaa za kijamii zilizotolewa na ujumbe wa Tanzania kwa jopo la wasuluhishi wa mgogoro huo jijini Maputo, nchini Msumbiji, hivi karibuni.

Alisema katika majibu hayo, ujumbe wa Tanzania ulieleza kuwa ushahidi wa kimazingira unathibitisha pasi na tone la shaka kwamba asilimia 60 ya ziwa hilo liko katika ardhi ya Tanzania.
Membe alisema uthibitisho wa hilo ni kuwapo mabaki ya nyumba, shule, miti ya miembe na makaburi ya mababu za baadhi ya Watanzania wanaoishi mkoani Ruvuma kilomita tatu ndani ya ziwa hilo.
Membe alisema hoja hiyo ilitolewa na Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), John Komba, aliyekuwa katika ujumbe wa Tanzania, ambaye alisema makaburi hayo yamekuwa yakiwafanya wakazi wa Mbambabay, mkoani humo, kuwa na ada ya kwenda kufanya matambiko kila baada ya miezi mitatu kwa mwaka, ambako hukuta misalaba kwenye makaburi hayo.
Alisema dai hilo liliungwa mkono pia na ujumbe wa Malawi, ambao alisema walipoulizwa na jopo hilo, walikubali kuwapo na vitu hivyo ndani ya ziwa hilo.
Membe alisema majibu hayo yalitolewa baada ya ujumbe wa Tanzania kuulizwa sababu za Tanzania kutoa madai hayo hivi sasa, badala ya kufanya hivyo tangu miaka ya 1960, au 1970 au 1980 iliyopita.

0 comments:
Chapisha Maoni